Jumatano 13 Agosti 2025 - 10:00
Mtazamo juu ya jinai zinazofanywa na Israel dhidi ya waandishi wa habari

Hawza/ Mwishoni mwa siku ya Jumapili, shambulio la ndege isiyo na rubani kutoka Israel lililipua eneo la Hospitali ya Ash-Shifa na kulenga moja kwa moja hema la waandishi wa habari, baada ya msaada wa wananchi, ilibainika kuwa wafanyakazi watano wa Al Jazeera walikuwa wameuawa kishahidi, akiwemo Anas Ash-Sharif, moja ya sura mashuhuri katika taarifa za habari za Palestina na Ghaza.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha  Shirika la Habari la Hawza, Anas Ash-Sharif, mwenye umri wa miaka 28, mwandishi wa habari wa Al Jazeera eneo la Palestina, alikuwa miongoni mwa watu wanaotambulika sana kutokana na taarifa zake za kudumu kuhusu Ghaza.

Mwandishi mwingine wa Al Jazeera, Muhammad Qurayqah, mwenye umri wa miaka 33, alimaliza ripoti yake ya moja kwa moja ya mwisho kuhusu hali ya hewa, dakika chache tu kabla ya kuuawa kwake.

Ibrahīm Zahr, ambaye pia alikuwa mmoja wa wanakikundi hiki cha habari, alikuwa mpiga picha wa Al Jazeera, Ibrahīm, mwenye umri wa miaka 25, alijiunga na kundi hilo akitokea katika kambi ya wakimbizi ya Jabaliya, kaskazini mwa Ghaza, kundi hili la wanahabari lilikuwa katika hema lililokuwa karibu na Hospitali ya Ash-Shifa ili waweze kutoa taarifa za moja kwa moja kuhusu majeruhi na jinai za Israel, na pia kwa sababu mawasiliano ya intaneti katika eneo hilo yalikuwa imara zaidi, hata hivyo, Israel, kwa kulilenga eneo hili, iliwaua kishahidi.

Hani Ash-Shir, mwandishi wa habari wa Al Jazeera, akizungumza kufuatia kitendo hiki cha kinyama, aliripoti kuwa Israel, jioni ya Jumapili, ililenga hema la waandishi hawa wa habari kwa kutumia ndege isiyo na rubani, utawala huu katili pia ulianzisha mashambulizi ya mfululizo katika upande wa mashariki, na kulipa jina la “mkanda wa moto”.

Kwa masikitiko, utawala dhalimu wa Kizayuni katika kipindi cha miezi 22 iliyopita, umewaua waandishi wa habari wengi kwa kuwatuhumu kuwa ni wanachama wa makundi ya kijeshi.

Al Jazeera imelaani vikali mauaji ya wafanyakazi wake, na katika tamko ililolitoa, imewataja waandishi wa habari wa Ghaza kuwa “sauti ya mwisho iliyosalia Ghaza.”

Chanzo: Al Jazeera

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha